Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 29 August 2015

KAMA WEWE NI MPENZI WA KUNYWA MAJI YA MADAFU BASI JUA UNAZIPATA FAIDA HIZI ZA KIAFYA

Maji ya madafu ni yamekuwa yakijipatia umaarufusana katika mikoa ya ukanda wa pwani ya Tanzania.

Lakini licha ya kutumia kinywaji hicho kama kinywaji, pia husaida sana kuondoa kiu, maji ya madafu yana faida lukuki kwa afya ya mwanadamu.

Miongoni mwa faida za maji hayo ni pamoja na kuimarisha misuli na ubongo, huku pia yakitumika kuzuia upungufu wa maji mwilini.

Maji ya madafu yanasaidia kuzuia muonekano wa kizee (anti-aging) hususani pale linapotumika vyema mara kwa mara.

Pia maji ya dafu yanasaidia kuimarisha mfumo wa usagaji chakula tumboni. Maji ya madafu yanasaidia kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili.

Maji ya madafu yanasaidia kukukinga dhidi ya magonjwa ya moyo pamoja na presha.

Hali kadhalika maji ya madafu yana utajiri mkubwa wa virutubisho mbalimbali, huku yakiwa na kiasi kidogo cha kalori

Mbali na hayo, maji ya madafu ni msaada mkubwa katika kuimarisha mzunguko wa damu mwilini.


Kwa maelezo na ushauri unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0784 300 300, 0769 400 800, 0716 300 200 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment