Saturday, 22 August 2015

KUTANA NA HIZI FAIDA ZA MATUMIZI YA KARANGA


Karanga wengi wetu huwa tunakula kama kiburudisho tu tena ambacho hakina umuhimu sana kwa afya yetu.

Ukweli ni kwamba karanga si chakula cha kupuuza iwapo utajua faida zake kiafya.

Karanga ni miongoni mwa vyakula ambavyo ndani yake hupatikana mafuta mazuri aina ya 'monounsaturated fats' ambayo ni mazuri kwa afya. Hivyo watu ambao hutumia karanga mara kwa mara huwa katika nafasi kubwa ya kuepukana na magonjwa ya moyo.

Mbali ya kuwa na mafuta mazuri yanayotoa kinga kwenye mwili, karanga pia zinavirutubisho muhimu  vinavyotoa kinga ndani ya mwili 'antioxidants' hivyo ni vyema kula karanga mara kwa mara.

Faida nyingine ambayo huweza kupatika ndani ya karanga ni pamoja na kutoa kinga ya saratani ya tumbo, hii ni kwa sababu karanga ndani yake kuna virutubisho kama vile phytosterols, resveratrol pamoja na 'folic acid'

Hayo ni machache kuhusu karanga kwa maelezo au ushauri zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment