Saturday, 15 August 2015

KUTANA NA HUYU KIJANA MWENYE MIAKA 26 LAKINI UMBILE LAKE NI LA KITOTO KABISA!


Kwa kawaida watu wengi hutumia gharama nyingi wakiwa na malengo ya kujaribu kuzuia wasionekana wamezeeka.

Mfano wanawake wao huamua kujichubua ngozi zao kwa mikorogo na kununua madawa ambayo yamkini yatawarejeshea mvuto wao !

Kwa kina baba, wao hunyoa nywele zao zote na ikiwa hakunyoa wanajipaka rangi nyeusi angalau waonekana kuwa bado ni vijana au wanadai

Lakini kwa bwana mmoja mwenye umri wa miaka 26 hali yake ni tofauti sana kwani ana umri wa miaka 26 lakini maumbile yake ni sawa na mvulana mwenye umri wa miaka 10 !

Bwana huyo anaitwa Hyomyung Shin, kutoka Korea Korea Kusini ni mlevi, ana wachumba wa kike, anavalia nadhifu ila tu sauti yake ni sawa na ile ya mvulana ambaye hajabaleghe.

 Hali hiyo kwa Shina inasababishwa na kuwa na ugonjwa wa nadra sana unaoitwa, 'Highlander Syndrome'. Ugonjwa huu unamsababisha, mtu adumae palepale inapompata.Kwa mfano Shina amesalia kuwa na sura sauti na maumbile ya kijana mwenye umri wa miaka 10. Shin alizaliwa mwaka wa 1989.

No comments:

Post a Comment