Monday, 17 August 2015

LOWASSA:NIMESIKITISHWA SANA WATU KUPIGWA MABOMU

Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema , Edward Lowassa amesikitishwa sana na kitendo cha watu kupigwa mabomu jijini Mwanza alipokwenda kwa lengo la kujitambulisha.

Kufuatia hali hiyo Lowassa aliwataka Polisi kutoingilia mchakato wa uchaguzi na kutumiwa na CCM kupambana na wapinzani na kwamba wakiendelea watakuwa wanajitafutia tiketi ya kupelekwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu  (ICC) mjini The Hegue.

“Nimesikitishwa sana kuwa watu wamepigwa mabomu asubuhi. Mkiendelea na mchezo huu tukimaliza uchaguzi tutawapeleka The Hague mkakipate cha mtoto na huko hamtarudi tena,” alisema.

Pilikapilika za mapokezi ya Lowassa zilianza saa mbili asubuhi, baada ya maelfu ya wafuasi wa Ukawa kutanda kwenye barabara inayoelekea uwanja wa ndege wakiwa na mabango yenye jumbe mbalimbali.

Lowassa aliwasili akiwa ameambatana na mgombea mwenza, Juma Duni Haji, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia, Kaimu Mwenyekiti wa CUF, Twaha Taslima na Mwenyekiti wa NLD, Dk Emmanuel Makaidi.

Mabomu ya machozi yalianza kurindima saa tano asubuhi, baada ya baadhi ya wafuasi wa Ukawa kutaka kuingia kwenye lango la uwanja wa ndege, huku wengine wakijaribu kuwatunishia misuli polisi kwa kuwatupia mawe.

Umati wa wafuasi wa Ukawa ukiwa katika Viwanja vya Furahisha jijini Mwanza jana walipohudhuria mkutano wa hadhara wa kumtambulisha mgombea urais kupitia Chadema, Edward Lowassa.
Katika hatua nyingine Lowassa katikati ya hotuba yake kwa wakazi wa Mwanza alisema anawasikitikia wale wanaobeza nguvu ya umm.
“Haya siyo mapenzi, haya ni mahaba. Wanaobeza nguvu hii ya umma nawatakia kila la heri,” alisema Lowassa huku akishangiliwa n umati wa watu.

Aidha, kwa upaande wa mke wa mgombea huyo Regina Lowassa alisema haijawahi kutokea maeneo yote waliyotembelea Dar es Salaam, Mbeya na Arusha.
“Mwanza nimewapenda, nafikiri baba (Lowassa) akitoka hapa atalala usingizi mzuri mzito,” alisema Regina.

No comments:

Post a Comment