Tuesday, 18 August 2015

MAJANI YA UKWAJU NA UWEZO WAKE WA KUTIBU KIKOHOZI

Majani ya ukwaju ni dawa
Je, umewahi kusumbuliwa na kikohozi kwa muda mrefu, licha ya kuwa hauna tatizo la kifua kuu lakini bado ukajikuta hakiponi? kama jibu ni ndio hebu jaribu tiba hii pia.

Tafuta majani ya ukwaju kiasi cha fungu moja la mboga za majani, kisha yatwange halafu weka maji robo lita katika majani hayo yaliyotwangwa na kisha koroga vizuri.

Ukishapata mchanganyiko huo, utahitajika kutafuta asali  kwenye ujazo wa kikombe kidogo cha chai kisha changanya na ule mchanganyiko wa majani ya ukwaju uliyoyasaga hapo awali kisha changanya vizuri na asali hiyo na uanze kwa kutumia kwa kunywa asubuhi na jioni kiasi cha kijiko kikubwa cha chakula. Unaweza kutumia tiba hii kwa muda wa wiki mfululizo.
Asali
Angalizo:
Ukihitaji kutumia tiba hii ni vyema uhakikishe kwanza umeshawahi kupima kifua kikuu na ukagundulika huna tatizo,  kwani kikohozi cha muda mrefu ni moja ya dalili za kifua kikuu, hivyo kama ni kifuu kikuu ni vyema ukafuata ushauri wa daktari kwani dawa hii hutoa msaada kwa wale wenye kikohozi cha kawaida tu na si tiba ya kifua kikuu.

Ni vyema ukapata maelezo zaidi na ushauri kutoka kwetu kabla ya kutumia, wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment