Friday, 28 August 2015

MAMA REGINA LOWASA AWATAKA WANAO HOJI KUHUSU AFYA YA MUMEWE WAMUULIZE YEYE

Mke wa Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa , Mama Regina Lowassa akiongea na wanawake wa CHADEMA katika ukumbi wa Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Wakati kukiwa na taarifa nyingi mchanganyiko kuhusu afya na uadilifu  wa mgombea urais kwa tiketi ya UKAWA Edward Lowassa, hali hiyo imesababisha mke wa mgombea huyo Regina Lowassa kuibuka na kusema kwamba wenye maswali kuhusu mumewe wamuulize yeye.

Hayo aliyasema wakati akizungumza katika kongamano la Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha) nakusema kwamba anawashangaa watu wanaotunga uongo dhidi ya mumewe, huku akijiuliza kwanini watu watunge uongo huo wakati yeye yupo.

"Najiuliza hivi kwanini watu watunge vitu vingi vya uongo juu ya mtu huyu (Lowassa)  wakati mimi nipo?" alisema Regina huku akishangiliwa na umati wa wanawake 

Akielezea sifa za mume wake mama Regina Lowassa alisema mume wake ni mchapakazi, huku akiwaomba wanawake kumchagua.

No comments:

Post a Comment