Friday, 21 August 2015

MANENO YA JAMES MBATIA WA UKAWA KUHUSU KUZUIWA KUTUMIA UWANJA WA TAIFA PAMOJA NA DK, SLAA KUENDELEA KUTOONEKANA

James Mbatia (picha kwa msaada wa mtandao)
Umoja wa UKAWA walihitaji kuutumia Uwanja wa Taifa kwenye uzinduzi wa Kampeni zao, lakini hawakupata ruksa hiyo.

Agosti 20, 2015 James Mbatia ambaye ni mmoja wa viongozi wa umoja wa UKAWA, amekutana na waandishi wa habari kwenye Ofisi za Makao Makuu ya NCCR- Mageuzi, Ilala Dar es Salaam na kulizungumzia suala hilo.

Katika mazungumzo yake na waandishi wa habari, Mbatia amezungumzia kuhusu kufanya kampeni za kistaarabu na swala la kuendelea kutoonekana kwa Dk Wilbroad Slaa.

“Kampeni zinaanza nawasihi wanasiasa wote wachunge ndimi zao sana, tujadili hoja kwa hoja kwenye majukwaa ya kisiasa sio kujadili watu, matusi, wala kupigana ngumi au kumwaga damu" alisema Mbatia

Pia Mbatia ameitaka Tume ya Uchaguzi pamoja na vyombo vya dola kutenda haki ili kuepusha migogoro.

"Tume ya Uchaguzi ambayo ndio refa itende haki pamoja na vyombo vya dola… Wakitenda haki hakuna mgogoro wa aina yoyote, Kamati za Ulinzi na Usalama Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya hatutaki waingilie mchakato huu"

Kwa upande wa ishu ya kuzuiwa kutumia Uwanja wa Taifa Mbatia alisema “Uwanja wa Taifa ni mali ya Watanzania, tutakutana tutatafakari alafu tukishakubaliana kwa pamoja tutatoa taarifa wapi tutakutana na tutazungumza nini, kwa kweli hatuna majibu mpaka sasa hivi“

Kuhusu swala la Dk. Slaa kutoonekana kwenye vikao vya UKAWA Mbatia alisema “UKAWA sio Mbatia, sio Slaa sio Lipumba sio Mbowe… tusijadili watu tujadili hoja za msingi za taifa, watu wanapita, tuzungumzie Watanzania zaidi“

Unaweza kuisikia sauti ya James Mbatia hapa chini akiyaelezea hayo yote>>>

No comments:

Post a Comment