Monday, 3 August 2015

MATATIZO AMBAYO HUWEZA KUAMBATANA NA KUKOMA KWA HEDHI (MENOPAUSE)

Katika umri fulani wa mwanamke  hasa kuanzia miaka 45 na kuendelea (kutegemeana na mwanamke) hedhi hukoma.(menopause)

Baada ya kukoma huko kwa hedhi shughuli zote za uzazi kwa mwanamke nazo hukoma.

Wanawake wengi wengi hujikuta wakati wao wa hedhi kukoma ukifika bila hata kuona dalili zozote za awali kwa wengine huchukua hadi mwaka mmoja kwa kuambatana na matatizo ya aina mbalimbali.

Hali hii ya kukoma kuingia hedhini huweza kusababisha matatizo yafuatayo kwa mwanamke husika:

  1. Kukosa hamu ya chakula.
  2. Kuhisi njaa kupita kiasi.
  3. Kupata maumivu ya mgongo na kuumwa kichwa mara kwa mara.
  4. Kupungua uzito.
  5. Kuhisi kizunguzungu.
  6. Maumivu ya maungo yote mwilini.
Matatizo yanayotokana na hali hii huwa hayana tiba kamili, lakini ni vyema mhusika aikubali hali halisi na ikiwezekana kumwona daktari mara tatizo linapoonekana kuzidi.

Kwa ushauri zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 barua pepe dkmandatz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment