Tuesday, 4 August 2015

NAPE ALIHUSISHWA NA SUALA LA RUSHWA HAPA KAAMUA KULITOLEA UFAFANUZI SWALA HILO(AUDIO)

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amesema amesikitishwa namna vyombo vya habari vinavyoripoti suala la rushwa kwenye chaguzi za kura za maoni.

Aidha, Nape amesema ni vizuri haki ikatendeka wakati wa kuripoti mambo hayo, huku akisema kuwa suala la kuripoti kuwa yeye alihojiwa na TAKUKURU kwa masaa matano lilikuwa si la kweli na kusema huo ni uongo mkubwa mchana kweupe na hata TAKUKURU walipotoa maelezo ya kweli juu ya swala hilo vyombo vya habari havikuripoti suala hilo

"Walikuwa nauwezo wa kubalance lakini wakaamua kuandika stori ya uongo, mimi mwandishi wa habari na najua utaratibu wa kuandika stori walikuwa na uwezo wa kunipata, lakini kwa sababu walikuwa wameamua kuandika uongo wenye lengo la kumchafua Nape wakaona tukimpata Nape stori yetu itakufa wakaamua kuibeba kama ilivy".  Alisema Nape


Katika hatua nyingine Nape amesema "hii ni aibu kwa tasnia ya habari na mimi nadhani wanahabari imefika wakati tulaani matendo ya namna hiyo"

Kama unahitaji kupata undani zaidi kuhusu ufafanuzi huo msikiliza Nape mwenyewe hapa chini akizungumzia suala hili kwa undani zaidi.>>Tunapenda kukukaribisha sana kutangaza nasi kwa matangazo mbalimbali wasiliana nasi sasa kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300 0769 400 800 email dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment