Tuesday, 11 August 2015

PATA NAFASI YA KUFAHAMU JINSI YA KUTUMIA KITUNGUU MAJI KWA KUKUZA NYWELE ZAKO

Kuna msemo wa kinadada hupendelea kusema kwamba 'mwanamke nywele', lakini wengi hukubwa na changamoto za kutokuwa na nywele nzuri na zenye afya.

Ni kweli kwamba moja ya urembo wa kinadada na kinamama ni pamoja na muonekano wa nywele nzuri na ndio maana leo nimeona nikusogezee hii mbinu nyingine ya kukuza nywele.

Kitunguu ni moja ya kiungo kizuri ambacho kinauwezo wa kufanya nywele kuweza kukua vizuri na kuwa na afya endapo kikitumika inavyopaswa.

Kitunguu kinapotengenezwa juisi na kutumika kupaka kwenye nywele husababisha matokeo mazuri sana kwa nywele.

Jinsi ya kuandaa 
Utapaswa kupata vitunguu vitatu au vinne kisha vioshe vizuri halafu kata vipande vidogo vidogo ndani ya  brenda kisha saga.

Baada ya kupata juisi yake tumia juisi hiyo kwa kupaka kichwani huku ukihakikisha inafika kwenye mizizi ya nywele kabisa yaani hadi usawa wa kichwa.
Ukishapaka subiri baada ya saa moja kisaha osha kichwa chako kwa maji safi. Fanya zoezi hili kwa mda wa mwezi mmoja utaona mabadiliko.

Kwa ushauri zaidi wasiliana nasi kwa  simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pep dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment