Wednesday, 26 August 2015

POLISI YAMUONYA LOWASA WASEMA STAILI YA KAMPENI ZAKE INAWEZA KUTUMIWA NA MAADUI WA KISIASA KUMDHURU


Jeshi la polisi kanda Maalum ya Dar es Salaam limemtahadharisha mgombea wa urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa kuwa kampeni alizozianza za  kutembelea makundi kadhaa zinaweza kutumiwa na maadui wa kisiasa kumdhuru.

Kauli hiyo inafuatiwa ikiwa ni siku mbili tangu Lowassa na mgombea mwenza Juma Duni Haji walipoanza kuwatembelea wananchi kwa kutumia usafiri wa umma.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova amesema ziara iliyofanywa jana na mgombea huyo maeneo ya Swahili, Kariakoo zimechangia mikusanyiko isiyokuwa yalazima na kusababisha shughuli za maendeleo kusimama.

Hata hivyo, wanasiasa wametakiwa kufuata ratiba ya kampeni kwa kuzingatia mwongozo wa Tume ya Uchaguzi (NEC) ili kulisaidia Jeshi la Polisi kukabiliana na vitendo viovu.

Karibu utangaze nasi kupitia tovuti hii kwa gharama nafuu sana, tupigie simu sasa kwa namba zifuatazo: 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800.

No comments:

Post a Comment