Thursday, 6 August 2015

PROF: LIPUMBA ATANGAZA KUJIUZULU NAFASI YAKE YA UENYEKITI CUF TAIFA

Zilianaza kama tetesi sasa imekuwa rasmi ni baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba leo kutangaza kujiuzulu uenyekiti ndani ya chama hicho.

Akizungumzia sababu za kujiuzulu kwake, Profesa Lipumba amesema amekerwa na hatua ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ambao CUF ni chama shiriki kushindwa kusimamia makubaliano yaliyopelekea kuundwa kwa umoja huo.

Amesema Ukawa ulianzishwa kulinda maslahi ya wananchi yaliyoainishwa kwenye Katiba iliyowasilishwa kwenye Bunge Maalumu la Katiba, na kwamba nafsi yake inamsuta hivi sasa kuendelea na uongozi huku waliokuwa wanaipinga Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba wakikaribishwa kuwania uongozi wa nchi kupitia umoja huo.

Hivi sasa Prof. Lipumba amesema baada ya kujiuzulu atajikita kufanya shughuli za kitaaluma kwa kujihusisha zaidi na ushauri wa masuala ya uchumi na maendeleo.

No comments:

Post a Comment