Tuesday, 25 August 2015

SABABU HIZI ZITAKUFANYA UENDELEE KULIPENDA TANGO

Tango ni miongoni mwa matunda ambayo yanaelezwa kuwa na faida mbalibali kwa afya licha ya kwamba tunda hili huwa halina ladha ya utamu, lakini uzuri wake unakuja kwenye faida zake zaidi.

Leo ninazo baadhi ya faida za tunda hili zipitie hapa chini>>

Kwanza kabisa tunda hili hutumiwa sana kuleta uzuri na kuimarisha afya ya ngozi kwa kusugulia uso kwa kipande cha tango, unachopaswa kufanya ni kuosha uso kwa juisi yake na utaona mabadiliko.

Husaidia sana kusafisha  au kuzuia magonjwa ya ini na magonjwa ya figo pamoja na koo.

Juisi yake pia husaidia mwili kufanya kazi yake vizuri inapotumika kwa kunywa.


Kwa wale wenye shida ya mikono yenye kuchubuka na iliyokauka wanashauriwa kutumia tango kwa kupaka mikono (kuoshea)  au kupaka mwili wote.

Husaidia kuondoa chunusi na michubuko ya mwili n.k

Halikadhalika tango pia ni msaada kwa wale wenye kusumbuliwa na kisukari na wa kupunguza uzito wa mwili hutakiwa kulifanya tunda hili kuwa sehemu ya mlo wao.
 
Tango pia huondoa 'uric acid' ndani ya mwili

Kwa maelezo na ushauri zaidi tutafute kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment