Friday, 14 August 2015

SABABU ZA KUPATA MAUMIVU WAKATI WA TENDO LA NDOA

Maumivu wakati wa tendo la ndoa ni moja ya tatizo ambalo huwasumbua wanawake wengi, maumivu hayo hutokana na matatizo ndani ya kizazi. 

Tatizo hili huweza kutokea wakati wa tendo au baada ya kumaliza tendo. Maumivu ya wakati wa tendo mara nyingi huchangiwa na maambukizi ukeni yanayosababishwa na magonjwa ya ngono na fangasi.

Maumivu pia hutokea endapo mwanamke ataumia sehemu zake za siri na kukutana na mwanaume basi huwa kunauwezekano mkubwa wa mwanamke kupatwa na maumivu hayo.

Mwanamke mwenye shida hii hupata maumivu makali wakati wa tendo na hata kushindwa kufurahia  tendo.

Baadhi ya wanawake wao wakipaliza tendo huhisi maumivu na muwasho au kama amepata majeraha ya wembe ukeni.

Tatizo la maumivu ndani ya kizazi au baada ya tendo la ndoa husababishwa na maambukizi katika viungo vya uzazi. Pia maambukizi huleta athari ambazo ni mirija ya mayai kuvimba au kujaa maji au usaha. 

Madhara ya tatizo hili ni ugumba kwani mirija inaweza kuziba kabisa au mayai yasizalishwe, siku kuvurugika na kupata maumivu wakati wa hedhi, lakini ni vema uwahi hospitali kwa uchunguzi wa kina.

Kwa ushauri zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment