Monday, 17 August 2015

SABABU ZA TATIZO LA KUKOSA CHOO, DALILI NA TIBA YAKE VYOTE VIPO HAPA
'Constipation' ni hali ya haja kubwa inayopatikana kwa shida mara zisizozidi 3 katika wiki au ile haja kubwa inayoleta shida katika upatikanaji wake.

Hali hiyo ya kufunga choo hutokea iwapo utumbo mkubwa utashindwa kufanya kazi yake kikamilifu.

Miongoni mwa vyanzo vya tatizo hili ni pamoja na kutokunywa maji ya kutosha, kula vyakula bila mpangilio maalum, utumiaji wa holela wa madawa, kula vyakula vilivyokaangwa mara kwa mara pamoja na kula kupita kiasi.

Pia dalili za tatizo hizo ni pamoja na kutopata choo mara kwa mara, kpata haja ambayo ni ngumu sana, kukosa hamu ya chakula, kuumwa kichwa na kuhisi kizunguzungu.

Papai moja ya tiba ya tatizo hili la kukosa choo
Dalili nyingine ni kuumwa mgongo, kiungulia, na kukosa usingizi.

Ili kukabiliana na shida hii unaweza kula kipande cha papai kila asubuhi hadi pale utakapoona mabadiliko ya kiafya.

 Unaweza kuwasiliana nasi kwa namba za simu zifuatazo 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment