Monday, 17 August 2015

SAFARI ZA MABASI YAENDAYO KASI KUANZA LEO JUMATATU ASUBUHI JIJINI DSM

Mabasi yaendayo kasi yalisubiriwa kwa muda mrefu sana na hatimaye sasa leo Jumatatu ya Agosti 17 mabasi hayo yataanza kazi kuanzia saa 3 asubuhi nje ya kituo cha Mabasi yaendayo Mikoani Ubungo.

Uzinduzi wa safari za mabasi hayo utaanza kwa kutoa huduma ya mpito na baadaye wananchi wataruhusiwa kupanda mabasi hayo kutoka Ubungo kwenda Kimara na kutoka Kimara hadi Kivukoni bure.

Deusi Dedith Mutasingwa ambaye ni Afisa wa masuala ya fidia katika mradi wa mabasi haya yaendayo haraka yaliyo chini ya ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na serikali za mitaa,amesema yapo mabasi ya aina mbili kuna yale ya mita 18 ambayo yana uwezo wa kubeba abiria 140 na yapo yenye uwezo wa kubeba watu 80.

Mbali na hayo, amesema mabasi hayo pia yamezingatia watu wenye mahitaji maalum kama walemavu na wajawazito.

Hata hivyo kufuatia uzinduzi huo wafanyabiashara wanaopanga vitu vyao pembeni ya barabara na kwenye vituo wameombwa kuviondoa na kwa wale watakaonekana kukaidi amri hiyo faini yake si chini 250,000.

No comments:

Post a Comment