Saturday, 15 August 2015

SIFA ZA MATUMIZI YA MAFUTA YA MZAITUNI


Habari za leo mdau wangu wa www.dkmandai.com bila shaka unaendelea vizuri na majukumu yako ya kila siku.

Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa wewe ambaye umekuwa ukituma maswali yako kupitia barua pepe yetu na ukurasa wetu wa facebook pamoja na ujumbe mfupi wa maneno kupitia simu.

Leo napenda kujibu moja ya swali la mdau ambaye yeye alihitaji kufahamu faida za matumizi ya mafuta ya mzaituni

Miongoni mwa faida za mzaituni ni pamoja na kusaidia sana kulainisha ngozi, pia yana kiasi kikubwa cha vitamin A, D, E na K ambazo husaidia sana kuondoa sumu kwenye ngozi, hivyo matumizi ya mzaituni yataifanya ngozi yako kuendelea kuonekana nyororo na yenye afya zaidi.

Mafuta haya ya mzaituni yanauwezo wa kusaidia kutuliza maumivu ya tumbo pia husaidia sana kutibu tatizo la mafua ambapo mhusika atapaswa kupaka kati ya tundu moja la pua na jingine mara tatu kwa siku.

Kwa wale wenye shida ya ganzi miguuni au mikononi huweza kutumia mafuta haya ya mzaituni kwa kuchua sehemu zote zenye shida, tumia kwa kuchua asubuhi na jioni.

Matumizi ya mzaituni katika chakula husaidia sana kupunguza uzito kwa watu wenye uzito mkubwa

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com. Pia unaweza kututafuta kupitia ukurasa wetu wa facebook uitwao Mandai Herbalist Clinic-mhc kisha like hiyo page na utaweza kuuliza maswali yako kupitia inbox yetu

No comments:

Post a Comment