Wednesday, 5 August 2015

TFDA YATOA IDADI NA THAMANI YA VIPODOZI VILIVYOTEKETEZWA 2014/ 2015Suala la upigaji marufuku wa vipodozi visivyo salama kwa afya ya watumiaji si geni hapa nchini limekuwa likielezwa mara kwa mara.

Kufuatia hali hiyo Mamlaka ya chakula na Dawa TFDA imetoa ripoti ya mwaka wa fedha kuhusu bidhaa mbalimbali zilizokamatwa na kuteketezwa kwa mujibu wa sheria na hatua zilizochukuliwa.

Akitoa ripoti hiyo Mkurugenzi wa TFDA Hitti Sillo amesema katika mwaka wa fedha wamekamata na kuteketeza vipodozi ambavyo vimepigwa marufuku tani 16.61 ambazo thamani yake ni shilingi milioni 44.2.

‘Vipodozi ambavyo vimepigwa marufuku vilivyoingizwa tumekamata vikiwa vinaingizwa nchini na vingine vimekutwa katika soko vikiwa tayari vimeingizwa na vingine vikiwa njiani kuingizwa nchini, mara nyingine tumekamata mabasi yakiwa na vipodozi vinavyoingizwa nchini kinyume cha sheria vyote hivyo thamani yake kwa mwaka wa fedha uliopita ni shilingi milioni 44″ Sillo.

Aidha, Sillo amesema kazi hiyo ni endelevu kwa kuwa TFDA ipo sehemu mbalimbali nchini na wakaguzi wake wapo kuanzia bandarini na katika viwanja vya ndege ambapo ndipo hukamataa bidhaa nyingi.

Katika hatua nyingine Sillo amesema miaka mitatu iliyopita udhibiti umeimarika sana ndio maana matukio mengi ya kukamatwa kwa watu ambao wanaingiza vipodozi hatari kinyume cha sheria wanakamatwa wakiwa mipakani.

Asante kwa kufuatilia tovuti yetu hii, lakini kumbuka kuwa endapo unasumbuliwa na magonjwa sugu unaweza kuwasiliana nasi Mandai Herbalist Clinic kwa simu zifuatazo ; 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment