Thursday, 27 August 2015

TUMIA FURSA HII KUFAHAMU HUU UMUHIMU WA MBEGU ZA HAYA MABOGA KWA AFYAMaboga hutokana na tunda liitwalo boga, tunda ambalo asili yake haifahamiki vizuri ni wapi, ingawaje baadhi ya tafiti zinasema kuwa asili yake ni Amerika ya kaskazini.

Zao la maboga mara nyingi hushamiri zaidi katika msimu wa joto na inashauriwa kupanda zao hili mwanzoni mwa mwezi Julai hasa katika udongo unaotunza maji vizuri.

Hata hivyo, zao hili huweza kuathirika endapo kutakuwa na upungufu wa maji au joto dogo sana, lakini pia zao hili huweza kuathirika linapopandwa katika udongo ambao hauchuji maji vizuri.

Mbegu za maboga zinafaida nyingi sana kiafya na hujumuisha kiwango kingi cha protini na vitamin, huku ikiaminika kwamba, mbegu hizo huweza kupunguza mafuta kwenye mishipa ya damu na jambo la msingi zaidi ni kwamba gramu moja ya mbegu za maboga huwa na protini sawa na glasi moja ya maziwa.

Watu wengi wanaweza kudharau mbegu za maboga pengine kwa kutokufahamu faida zake, lakini wazi kwamba mbegu hizi ni miongoni mwa mbegu zenye faida kubwa mwilini, kwani huweza kuzuia na kutibu hata baadhi ya magonjwa hatari yaliyoshindikana hospitalini.

Miongoni mwa faida za mbegu hizi ni pamoja na kuimarisha mifupa na moyo, hii ni kutokana na kuwa na kiwango kingi cha madini aina ya magnesium, ambayo ni muhimu kwa afya ya moyo na uimarishaji wa mifupa pamoja na mishipa ya damu.

Aidha, mbegu hizi za maboga pia zina kiwango cha madini aina ya 'zinc', ambayo faida yake mwilini ni pamoja na kuimarishaji kinga mwilini , Hali kadhalika zinc huimarisha nguvu za kiume.

Kutokana na kuwa na kiwango kingi cha zinc, tafiti zinaonesha kuwa mafuta ya mbegu zenyewe za maboga huweza kutumika kama dawa ya kutibu saratani ya kibofu.

Mbali na hayo mbegu hizi zina virutubisho vinavyotoa kinga dhidi ya magonjwa ya ini na moyo.

Pamoja na hayo, pia wale wenye shida ya kukosa usingizi au kuwa na usingizi wa mang’amung’amu wanashauriwa kula punje kadhaa pamoja na tunda lolote muda mfupi kabla ya kupanda kitandani, utafiti umeonesha kwamba mbegu za maboga zina kirutubisho kinachohamasisha uzalishaji wa homoni za usingizi kwa wingi

Halikadhalika mbegu za maboga zina virutubisho vingi vyenye uwezo wa kuzuia magonjwa yote ya uvimbe mwilini, ikiwa ni pamoja na kuvimba miguu, vidole na hata majipu.

Hakikisha unakula mbegu ambazo hazijaoza na zilizo safi na ambazo hazijakaa muda mrefu, lakini pia tumia mbegu hizo kwa usalama zaidi ikiwa ni sambamba na kuziosha na maji safi na salama kisha zianike na inapendeza zaidi ukila bila kukaanga, lakini ukila pia baada ya kukaanga bado utapata faida zake. Isipokuwa hakikisha haziungui wakati unapozikaanga unaweza kutumia dakika 10 tu katika zoezi hilo la kuzikaanga.

Kwa maelezo zaidi au ushauri tupigie simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com facebook Mandai Herbalist Clinic - mhc. Tunapatikana Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment