Tuesday, 25 August 2015

TUMIA MBEGU ZA PARACHICHI KUTIBU MAUMIVU MAKALI WAKATI WA KUTOA HAJA NDOGO (PAINFUL URINATION)Habari za leo Jumanne ya Agosti 25, 2015 mdau wangu wa www.dkmandai.com bila shaka unaendelea vyema kabisa na majukumu ya kila siki, lakini kama haupo vizuri basi naomba nitumie fursa hii kukupa pole, lakini ni kusihi usikate tamaa ndugu yangu zidi kumuomba Mungu tu kwahayo magumu unayopitia atakusaidia.

Baada ya kuyasema hayo naomba nizungumzie kile nilichodhamiria kukufikishia kwa sasa na si kingine bali ni hili tatizo la kupata haja ndogo (mkojo) yenye kuambata na maumivu makali na kutoka kwa taabu sana.

Hii shida imekuwa ikiwakumba wengi kwani nimekuwa nikipokea maswali ya nanma hii mengi na wengi wakiomba kufahamu namna ya kukabiliana na shida hii.

Kimsingi ni kwamba kupata maumivu wakati wa haja ndogo ni moja ya dalili kuwa huenda unatatizo la  U.T.I ikiwa na maana kwamba umepata madhara kwenye mfumo wako wa njia ya mkojo. Jambo ambalo hukosesha raha kabisa wakati wa utokaji wa haja hiyo na hufika wakati hata kutotamani kupata haja hiyo ndogo kabisa.

Pia maumivu haya ambayo hujitokeza wakati wa kukojoa huweza kuwa ni dalili za tatizo la tezi dume
'prostatitis', kisonono 'gonorrhe' pamoja na matatizo ya mawe kwenye figo 'kidney stones'

Hivyo moja ya njia ya kawaida kabisa ya kujaribu kuondoa shida hii ni kuhakikisha unakunywa maji ya kutosha angalau lita 4 kwa siku hii itakusaidia sana kumaliza shida hiyo.

Sasa endapo ukajitahidi kunywa maji ya kutosha na bado tatizo likaendelea basi ni vyema utumia tiba hii ifuatayo:

Tafuta mbegu au peke la parachichi  'avocado seed' na ulisage kisha kaanga kiasi , baada ya hapo utatumia unga huo kwa kuweka vijiko viwili vya unga huo kwenye kikombe chenye maji ya moto na kukoroga vizuri  kisha kunywa maji hayo. Fanya hivyo kwa muda wa siku 10
Mbegu ya parachichi
Dawa hii itakuwa msaada sana kwako wewe mwenye shida ya kukwama kwa mkojo au kupata haja ndogo yenye maumivu makali.

Hata hivyo, ukiona hali inaendelea ni vyema kuoaana na daktari wako kwa ushauri zaidi au wasiliana nasi Mandai Herbalist Clinic kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300, 0653 163 838 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com au fika kituoni kwetu tupo Ukonga, Mombasa maeneo ya Mongolandege jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment