Saturday, 8 August 2015

TUMIA MBINU HII KAMA UNAHITAJI KUACHA KUVUTA SIGARA


Uvutaji wa sigara ni moja ya mambo ambayo huwaathiri watu wengi kiafya , licha ya kuwa na madhara makubwa ikiwemo kuathiri uwezo wa mapafu katika utendaji kazi wake.

Watu wengi wanaovuta sigara ukijaribu kukaa nao na kuwauliza juu ya tabia hiyo wengi watakujibu kuwa wanavuta, lakini si kwamba wanapenda sana na wamekuwa wakijaribu kuacha lakini imeshindikana.

Sasa leo nimeona ni vyema tujuzane hii mbinu ambayo huenda itakusaidia kumaliza hamu na matamanio ya kuvuta sigara endapo ukiamua kuitumia.

Ili kumaliza tabia hiyo jitahidi upate kijiko kimoja cha baking soda kisha weka kwenye glasi yenye maji, kisha tikisa vizuri ili ichanganyike vyema na kuyeyuka kabisa.

Baada ya hapo utakuwa unakunywa mchanganyiko huo mara mbili kwa siku asubuhi na jioni na ukiona bado utaanza kutumia tiba hiyo mara moja kwa siku.

Lakini pia unaweza kutumia maji yenye mchanganyiko huo kwa kusukutulia mdomo kila unapohisi hamu ya kuvuta sigara. Hivyo unaweza kutembea na maji hayo kwenye chupa ya maji ili utumie pale unapohisi kuvuta sigara.

Karibu sana Mandai Herbalist Clinic upate suluhisho la magonjwa sugu tiba zetu ni za mimea, matunda, nafaka na mitishamba tunafanya kazi kila siku Jumatatu hadi Jumapili. Kumbuka kuwa tunapatikana Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam na kwa mawasilano zaidi tutafute kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800, 0652 163 838 barua pepe ni dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment