Friday, 21 August 2015

TUMIA TANGAWIZI ILI KUEPUKA MAUMIVU MAKALI WAKATI WA HEDHI


Tangawizi tumekuwa tukiwa nayo karibu kila siku katika maisha yetu ya kawaida na mara nyingi wengi wetu huitumia kama kiungo kwa ajili ya kuleta harufu nzuri kwenye chai.

Lakini kimsingi ni kwamba tangawizi huwa na nafasi kubwa na nzuri ya kutumika kama tiba na kuondoa aina mbalimbali za vikwazo katika afya yako.

Moja ya shida ambayo huweza kupata suluhisho kutokana na matumizi ya kiungo hiki (tangawizi) ni pamoja na tatizo la wanawake kuhisi maumivu makali wakati wanapoingia kwenye siku zao 'period.'

Wengi hulalamika sana kwa kuhisi maumivu chini ya kitovu au maumivu makali ya kiuno, lakini kumbe tangawizi inaweza kuwa msaada katika swala hili.

Jambo la kufanya ni kupata tangawizi kisha utaisaga na kupata unga wake halafu utakuwa maji yenye mchanganyiko wa unga huo wa tangawizi na baadaye utakunywa.

Ili kuzuia maumivu hayo utapaswa kunywa siku tangawizi kila siku kikombe kimoja siku  3 kabla yakuanza kuziona siku zako, kwa kufanya hivyo itakusaidia sana kuondoa maumivu hayo ya hedhi.

Mbali na hayo, tangawizi husaidia sana kuimarisha afya ya mwili na kuzuia kichefuchefu kwa wale wenye kutapika pamoja na kuongeza hamu ya kula 'appetite' kwa wenye shida ya kukosa hamu ya kula.

Kwa maelezo na ushauri zaidi wasiliana nasi Mandai Herbalist Clinic kwa namba za simu zifuatazo 0784 300 300, 0769 400 800, 0716 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment