Thursday, 13 August 2015

UFAHAMU KUHUSU HUU UGONJWA WA SUNZUA

Ugonjwa wa Sunzua ama 'warts' husababishwa na virusi aina ya Human Papilloma (HPV), ambavyo husambaa kutoka kwa mtu mmoja mpaka mwingine kwa njia ya kujamiiana kunakohusisha njia ya haja kubwa, uke au ngono ya mdomoni.

Zinaa ni miongoni mwa magonjwa ambayo yanaongezeka kila siku na sababu kubwa ni jamii kutokuwa na utaratibu wa kupima afya mapema na hivyo kuchelewa kupata matibabu sahihi. Matokeo yake ni kusababisha madhara makubwa.
Watu wengi ambao hupata ugonjwa huu mara nyingi huwa hawaoneshi dalili zozote.

Warts kwa jina jingine ni nyama zinazotokea sehemu za siri katika uume au uke au ndani ya uke pia katika haja kubwa sehemu ya pembeni au katika mashavu ya ukeni. Pia sunzua huweza kutokea pembeni mwa mdomo au katika ulimi.

Hata hivyo, inaelezwa kuwa asilimia kubwa ya watu wanaougua ugonjwa huo ni wanawake kutokana na maumbile yao.

Kwa upande wa mwanaume wao wanapata kutokana na michubuko na hivyo virusi hivyo huingia katika njia ya mkojo na mwanaume anaweza kumwambukiza mwanamke kwa kumwagia mbegu.

Kwa ushauri zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment