Sunday, 9 August 2015

UKWAJU UNAUWEZO WA KUKUTIBU PALE UNAPOTEGUKA

Habari za leo mdau wa www.dkmandai.com ikiwa leo ni Jumapili ya Agosti 09, 2015 ningependa tufahamishane kuhusu namna ya kujitibu mkono ulioteguka au kupata maumivu ya ndani kwa ndani.

Kama utakumbwa na tatizo hili itakulazimu uhakikishe unapata ukwaju pamoja na chumvi.

Kisha tengeneza juisi ya ukwaju hakikisha inakuwa nzito, kisha weka chumvi nyingi kiasi ndani ya juisi hiyo na uchanganye vizuri mchanganyiko huo.

Baada ya kuchanganyika vizuri utatumia mchanganyiko huo kwa kupaka ile sehemu yenye maumuvu (ile iliyoteguka) ukiwa kama unachua halafu kaa na mchanganyiko huo kwa muda wa sasa 3 hadi 4.

Baada ya muda utanawa kisha fanya hivyo asubuhi na jioni hadi pale utakapoona mabadiliko.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na Dk Abdallaha Mandai kwa simu namba 0784 300 300, 0716 300 200, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment