Wednesday, 19 August 2015

UMEIPATA HII TAARIFA YA KUHUSU DAWA YA KUONGEZA HAMU YA TENDO LA NDOA KWA WANAWAKE? NINAYO HAPA

Shirika la Dawa na Chakula nchini Marekani limeidhinisha matumizi ya dawa ya kwanza kabisa iliyoundwa mahususi kuwatibu wanawake ambao hawana hamu ya kufanya mapenzi.

Pamoja na kuidhinishwa kwa dawa hiyo, imeelezwa kwamba dawa hiyo itaambatana na onyo kali la kiafya kuhusu uwezekano wa mwanamke kupata madhara ikiwa ataimeza pamoja na pombe.

Mojawapo wa mashirika ya kutetea haki za wateja limeunga mkono hatua hiyo lakini Shirika lingine limesema dawa hiyo ni hatari kwa wanawake.

No comments:

Post a Comment