Friday, 14 August 2015

UMEISIKIA HII YA MTOTO WA MIAKA 11 ALIYEJIFUNGUA MTOTO


Matukio ya watoto kubakwa ni moja ya matukio ambayo yamekuwa yakiripotiwa sana hapa nyumbani Tanzania na duniani kwa ujumla.

Sasa huko nchini Paraguay kuna taarifa ya binti wa miaka 11 aliyedaiwa kubakwa na baba yake wa kambo amejifungua mtoto wake wa kike.

Hatua ya binti huyo kujifungua inafikia baada ya mamlaka nchini humo kumzuia kutoa mimba yake wakati wote wa  ujauzito wake.

Hata hivyo, madaktari katika mji mkuu wa Asuncion wamesema binti huyo na mtoto wake aliyejifungua kwa njia ya upasuaji wanaendelea vizuri.
Tukio hilo limesababisha utata mkubwa nchini Paraguay na katika mitandao ya kijamii, Paraguay ni taifa linaloamini zaidi katika Ukatoliki ambapo mwanamke anaruhusiwa kutoa mimba pale tu afya yake inapokuwa hatarini.

Inaelezwa kuwa binti huyo alibakwa alipokua na umri wa miaka kumi pekee na baba yake wa kambo mwenye miaka arobaini na miwili ambaye kwa sasa yupo rumande akisubiria kutajwa kwa kesi yake wakati huo huo baba huyo amekanusha kuhusika katika tukio hilo.

No comments:

Post a Comment