Saturday, 15 August 2015

UNAIFAHAMU HII MBOGA? INAITWA BROKOLI ZIPO HAPA FAIDA LEO


Brokoli hii ni mboga ambayo imekuwa ikipata umaarufu katika siku za hivi karibuni, kutokana na faida zake kiafya.

Miongoni mwa faida za mboga hii ya brokoli, kwanza unapokula mboga unaupatia mwili wako virutubisho vingi na inakiwango kidogo cha kalori.

Brokoli ni mboga yenye virutubisho vingi kama vitamin A, C, K, potassium, ufwemwili na lutein.

Pia mboga hii husaidia mfumo mzima wa neva na ubongo kufanya kazi inavyotakiwa na pia kuipatia nguvu misuli.

Hii mdio mboga ya brokoli
Brokoli inasadia pia msukumo wa damu kuwa vizuri na inapambana na sumu mwilini na kusaidia na kujenga mifupa.

Pia kula mboga hii husaidia chakula kusagwa vyema, kuzuia kukosa choo, kushusha sukari kwenye damu.

Hayo ni machache kati ya yale mengi kuhusu brokoli, lakini kwa ufahamu zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment