Saturday, 1 August 2015

UNDANI KUHUSU UGONJWA WA NGIRI


 Ngiri au 'Hernia' ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi  na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.


Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Tatizo la ngiri huweza kumpata mtu yeyote. Miongoni mwa sababu ambazo huweza kumfanya mtu apate ugonjwa wa ngiri ni pamoja nak Kuwa na uzito mkubwa wa mwili au kuongezeka uzito kwa ghafla, kazi ya kubeba au kunyanyua vitu vizito, tatizo la kukohoa au kupiga chafya kwa muda mrefu, ujauzito au matatizo yanayojitokeza kwa mwanamke wakati wa kujifungua.

Ngiri hutambuliwa kwa kutokea kitu kama uvimbe au kujaa katika eneo husika

Wengi wa waathirika wa tatizo hilo hufanyiwa upasuaji ili kurekebisha misuli au tishu zilizolegea.Pia inashauriwa kufanya mazoezi ili kupunguza uzito wako na kuweka utaratibu mzuri wa kula chakula kinachojumuisha mboga mboga au matunda yenye nyuzi nyuzi (fibers), hii husaidia  kuwa vizuri.

Kwa ushauri zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 barua pepe dkmandatz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment