Sunday, 16 August 2015

UPE MWILI WAKO AFYA KWA KUPENDELEA KUNYWA MAJI YAKUTOSHA KILA SIKU

Kunywa maji ni moja ya mambo muhimu sana kwa afya zetu wanadamu na hata wataalamu wa afya wanashauri kwa siku angalau mtu anywe maji lita nne kwa siku.

Hata hivyo, hali katika jamii ni tofauti kidogo kwani mtu yupo tayari kunywa soda nyingi au bia kuliko kunywa maji.

Wengi tunasahau kuwa maji ni muhimu zaidi kwa afya zetu na tunashauriwa kunywa unapoamka asubuhi kabla ya kusafisha kinywa.

Maji husaidia sana kuweka sawa mmeng'enyo wa chakula na hivyo kumsaidia mtu kupata choo vizuri na kuondokana na tatizo la kukosa choo.

Hivyo ni vyema ukayafanya maji kuwa kilevi chako kwani husaidia pia kunyevusha ngozi na kuifanya ngozi yako kuwa laini na ya kuvutia.

Kuna watu inaweza kuisha siku nzima bila kunywa maji hata kidogo kwa kufanya hivyo unahatarisha usalama wa afya yako kwani maji yanasaidia vitu vingi mojawapo ni kusafisha mkojo na kuepukana na magonjwa kama U.T.I.

Kwa ushauri na maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment