Thursday, 13 August 2015

USIKUBALI KUMALIZA SIKU YAKO BILA KUJIULIZA MASWALI HAYA MUHIMU

Ninachoamini ni kwamba kuanzia asubuhi hadi inapofika jioni basi hapo katikati huwa kuna mambo mengi unakuwa umefanya hadi siku inapokamilika.

Mambo hayo huweza kuwa mazuri na yenye kujenga, lakini pia kuna wakati yanaweza kuwa mabaya na yasiyo na manufaa, lakini Je, hivi huwa unajiuliza maswali haya kila siku inapokwisha?

1. Je, leo una nafuu yoyote kuliko siku ya jana? Kama ipo ni ipi?

2. Je, ni kitu gani kipya umejifunza katika siku husika?

3. Kuna maamuzi yapi mapya umeyafanya yenye dhamia ya kuboresha maisha yako?

4. Kuna chochote umefanya kwaajili ya watu wengine au dunia kwa ujumla. Kumbuka si lazima kila zuri likunufaishe wewe tu au ndugu zako tu.

5. Je, umemuudhi nani siku ya leo?

6. Je, nini umekifanya au kukiandaa kwaajili ya kesho?

7. Umetimiza kwa kiasi gani mipango yako uliyojiwekea hapo awali?

8. Umepanga kufanyaje ili kuboresha pale ulipoharibu leo?

9. Je, umeonesha upendo kwa kiasi gani kwa familia yako kwa ujumla? mzazi, mke, watoto au mpenzi.

10. Lazima ujiulize ni lipi limekukwaza  zaidi na kwanini limekukwaza

Mandai Herbalist Clinic ni kituo cha kutibu magonjwa sugu wasiliana nasi leo kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300. 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment