Thursday, 13 August 2015

USIKUBALI KUWA MTUMWA WA POMBE, TUMIA NJIA HIZI ILI UFANIKIWE KUACHA

Pombe ni moja ya kinywaji hatari kwa afya ya mwanadamu, licha ya kwamba ni kinywaji ambacho kina wapenzi wengi sana.

Ubaya wa pombe ni pale  unapoanza kuitumia huwa kuna ugumu wa kuiacha kwa ghafla na hapo ndipo wengi hupata shida sana pale wanapofikia maamuzi hayo ingawaje huwa wanatamani kuiacha.

Leo nimeona tujuzane hizi mbinu huenda zikawa msaada kwako na ukaweza kufanikiwa kuacha kunywa pombe na ukawa umeepuka madhara mengine ya kaifya na hata kiuchumi pia.

Ikiwa wewe ni mlevi wa siku nyingi unachopaswa kufanya ni kuanza kupunguza idadi ya bia ambazo huwa unakunywa kwa kila siku. Kam huwa unakunywa bia tano kwa siku basi punguza taratibu uanze kunywa tatu, baadaye mbili na hatimaye moja. Kamwe usiache kunywa bia kwa ghafla moja kwa moja.

Acha kuishi na aina yoyote ya kilevi (pombe) ndani ya nyumba yako, hii itakusahwishi kuendelea kutumia na itakuwa ngumu kwako kuacha kutumia.

Achana na mawazo kwamba wewe mwili wako hauwezi kuishi bila pombe, kumbuka kwamba hayo ni mawazo potofu na tambua kwamba wewe hukuzaliwa na pombe hivyo unaweza kuishi bila kunywa pombe pia.

Jena utaratibu wa kufanya mazoezi na hasa mazoezi hayo yafanye ule muda ambao ulikuwa ukiutumia kunywa pombe.

Zingatia mlo kamili na kupendelea kula matunda kwa wingi.

Ili usirudie tena kunywa pombe ni vyema ukumbuke yale mabaya yote yaliyowahi kukutokea wakati ukiwa umekunywa pombe hii itakufanya kuhisi maumivu na kuona kuwa pombe haifai tena katika maisha yako.

Hakikisha unawaambia ndugu, jamaa na marafiki juu ya huo uamuzi wako wa kuachana na pome ili pale watakapokuona umetumia tena wakuulize imekuaje tena.

Hizo ni mbinu ambazo nimependa kushare na wewe ambaye unatamani kuacha pombe, lakini imekuwa ni mtihani kwako hebu fanya hayo huenda utapata mafanikio katika suala hili.

Unaweza kuwasiliana nasi kwa namba zifuatazo: 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment