Wednesday, 5 August 2015

UTAFITI: KAMA WEWE NI MPENZI WA PILIPILI BASI JUA UNAJIONGEZEA SIKU ZA KUISHI DUNIANI


Wengi tunafahamu pilipili na baadhi wanaitumia pia katika kuongeza hali au hamu ya kula chakula zaidi, lakini huenda ulikuwa hujui kwamba matumizi ya pilipili huenda yakawa na faida ndani mwili wako.

Sasa kwa mujibu wa utafiti mmoja uliofanywa nchini China umebaini kuwa ukila chakula kilichotiwa viungo kila siku hususani pilipili utakuwaa unajiongezea maisha marefu.

Inaelezwa kuwa watafiti mjini Baijing walidadisi maisha na vyakula wanavyokula wenyeji nusu milioni katika kipindi cha utafiti cha miaka 7.

Utafiti huo ulibaini kuwa wale waliokula chakula kilichojumuisha pilipili walikuwa katika hali bora zaidi kiafya wala hawakuwa katika hatari ya kuaga dunia, huku hali yao ya siha ikionekana kutofautiana sana ikilinganishwa na wale ambao waliweka viungo katika vyakula vyao chini ya siku moja kwa juma .

Aidha, unaambiwa kwamba kiungo kinachopatikana katika pilipili, 'capsaicin' kinauwezo wa kupigana na seli zinazofanya mtu azeeke

Hata hivyo, watafiti wanasema kuwa utafiti huo ulikuwa wa ushahidi tu, lakini wakashauri utafiti zaidi ufanyika kwingineko ili kupata uhakika zaidi.

Karibu sana Mandai Herbalist Clinic upate suluhisho la magonjwa sugu tiba zetu ni za mimea, matunda, nafaka na mitishamba tunafanya kazi kila siku Jumatatu hadi Jumapili. Kumbuka kuwa tunapatikana Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam na kwa mawasilano zaidi tutafute kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800, 0652 163 838 barua pepe ni dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment