Thursday, 20 August 2015

UTAFITI: WANAOFANYA KAZI KWA SAA NYINGI WAKO HATARINI KUPATA KIHARUSI

Je, wewe huwa unafanya kazi kwa saa ngapi ndani ya siku?

Utafiti umeeleza kuwa watu wanaofanya kazi kwa saa nyingi wako hatarini kupata kiharusi, utafiti huo ulifanywa kwa zaidi ya watu laki tano.

takwimu zilizochapishwa kwenye jarida la kitabibu, Lancet, linaonesha kwamba upo uwezekano wa ongezeko la hatari ya ugonjwa huo kwa watu wanaofanya kazi zaidi ya muda wa kawaida.

Wataalam wanasema watu wanaofanya kazi kwa saa nyingi zaidi wawe na utaratibu wa kupima kiwango cha msukumo wa damu.

Wataalamu wanasema kufanya kazi kwa muda mrefu zaidi kuliko kawaida na kukaa kwa muda mrefu ni mbaya kwa afya na ongezeko la hatari ya kupata kiharusi.

Daktari  Mika Kivimaki kutoka chuo cha jijini London ameuambia Mtandao wa Habari wa BBC kuwa watu wanapaswa kuwa makini na afya zao, kuangalia mtindo wao wa maisha na kuhakikisha wanapima vipimo vya damu kuepuka shinikizo la damu.

Ikiwa ungependa kutangaza nasi Mandai Herbalist Clinic unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment