Wednesday, 26 August 2015

WAGONJWA WA MATENDE NA MABUSHA KUFANYIWA UPASUAJI MTWARA

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Dkt. Mwele Malecela
Wagonjwa wanaosumbuliwa na matatizo ya Matende na Mabusha katika manispaa ya Mtwara Mikindani, wameishukuru wizara ya afya na ustawi wa jamii kwa kuzindua kambi ya kufanyia upasuaji , kupitia mpango wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele.

Uzinduzi huo umefanyika jana katika hospitali ya rufaa ya Ligula mkoani humo ambapo wagonjwa wasiopungua 100 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji kupitia huduma zitakazotolewa na madaktari bingwa wa upasuaji kutoka hospitali ya taifa ya Muhimbili.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Uchunguzi wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Dkt. Mwele Malecela, amesema wizara ya afya imeweka mkazo katika mkoa wa Mtwara kwasababu umekuwa ni mkoa mmojawapo kati ya minne ya Tanzania ambayo inaongoza kwa kuwa na wagonjwa wengi wa matatizo ya mabusha.

Dkt. Mwele amewaomba wakazi wa Mkoa huo kujitokeza kwa wingi kushughulikiwa tatizo hilo kwa ni kubwa na lipo karibu kila mkoa licha ya kwamba  mkoa wa mtwara umekithiri, hivyo hatua hiyo itasaidia kutokemeza kwa kiasi kikubwa magonjwa hayo.

No comments:

Post a Comment