Wednesday, 26 August 2015

WAKAZI WA DSM NA MOROGORO WAENDELEA KUANDAMWA NA KIPINDUPINDU, SABA WAPOTEZA MAISHA WENGINE 230 WALAZWA

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii nchini imesema hadi sasa watu 7 wameshapoteza maisha kutokana na ugonjwa wa kipindupindu, huku wagonjwa 230 wakilazwa katika kambi mbali mbali katika mikoa ya Dar es Salaam na Morogoro.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijin Dar es Salaam Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid amesema kuwa kati ya wagonjwa hao 194 ni kutoka Dar es Salaam na 36 ni kutoka Mkoa wa Morogoro.

Aidha, Dkt. Seif amesema ili kupambana na ugonjwa huo serikali imewaagiza maafisa Afya wa Kata zote nchini kuhakikisha wanafanya ukaguzi wa afya katika kaya, shule na vyuo vyote nchini ili kuhakikisha mazingira yanakuwa safi muda wote huku kanuni zote za afya zikifuatwa.

Pamoja na hayo, Dkt. Seif ameongeza kuwa watashirikiana na Idara ya Maji ili kutibu vyanzo vyote vya maji pamoja na kuwataka wananchi wote kuweka mazingira ya vyoo hasa vya shimo katika hali safi, huku akiwataka mama lishe kuzingatia usafi. 


Unakaribishwa kutangaza nasi kupitia tovuti hii kwa gharama nafuu sana wasiliana nasi sasa kwa simu namba 0769 400 800, 0653 163 838 barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment