Saturday, 1 August 2015

WATANZANIA WATAHADHARISHWA KUHUSU HALI MBAYA YA HEWA

Mamlaka ya hali ya hewa nchini imewatahadharisha wananchi kuwa mabadiliko ya tabia nchi yanayotokana na uharibifu wa mazingira huenda yakasababisha hali mbaya ya hewa nchini na kukosekana kwa mvua kwa wakati.

Hali hii itasababisha kuwepo kwa hali mbaya ya chakula na ukosefu wa maji kwa muda mrefu katika maeneo kame.

Mkurugenzi wa utafiti wa mamlaka ya hali ya hewa nchini Ladislaus Chang’a amesisitiza kuwa iwapo wananchi hawatoweza kubadilika kitabia huenda nchi ikakumbwa na maafa makubwa yakiwemo ukosefu wa mvua hali mbaya ya hewa pamoja na majanga mengine yanayo sababishwa na uharibifu wa mazingira.

Ladislaus changa,amesema kuwa Tanzania ni miongozi mwa nchi zilizokumbwa na tatizo la mabadiliko ya tabia ya nchi jambo lililosababisha vifo vya watu kadhaa jijini dar es salaaam, hivi karibuni.

Akizungumzia athari zinazoweza kujitokeza kutokana na uihalibifu wa mazingira mkurugenzi huyo wa utafiti amesema kuwa,inawabidi wananchi kujifunza kutokana na mambo mbalimbali yaliyotokea hivi karibuni hapa nchini.

Wanafunzi wa chuo cha maendeleo ya jamii cha buhare na wanafunzi wa shule ya sekondari ya musoma utalii wamesema serikali inabidi ifanya jitihada za kukabiliana na hali hiyo na kuwapa taarifa mapema wananchi ili waweze kujiandaa kabla ya maafa hayajawakuta.

Mamlaka ya hali ya hewa nchini ipcc,imeanza kutoa elimu kwa wananchi ili kuweza kufahamu kuhusu mabadiliko ya tabia nchi yatokanayo na uhalibifu wa mazingira,ili kuweza kukabiliana na tatizo la uharibifu wa mazingira.


Source: STAR TV

No comments:

Post a Comment