Thursday, 6 August 2015

YAPENDE MACHO YAKO KWA KUFANYA HAYA ILI KUYALINDA YASIHARIBIKE.Jijengee utaratibu wa kufanya uchunguzi wa mara kwa mara wa macho ili kutambua kama utakuwa na magonjwa yanayoweza kusababisha upofu.

Epuka kufanya kazi zako sehemu ambayo itakuwa na mwanga hafifu hii itasababisha macho yako kutumia nguvu nyingi sana katika kuona.

Acha kuangalia moja kwa moja mwanga mkali kama jua au moto wa kuchomelea na kama utakuwa unafanya kazi kwenye kifaa kinachotoa mwanga ni vyema ukaa umbali wa sentimita 25 mpaka 30.

Zuia macho yako kwa miwani ya jua ukiwa unaendesha pikipiki, baiskeli hii itasaidia macho kutopigwa na vumbi au kuingiwa na wadudu machoni.

Kuna watu hupenda kusoma vitu, huku wakiwa wanatembee hii nayo si nzuri kwa afya ya macho.

Epuka kutumia taulo za kuogea kwa kushare, kwani ugonjwa wa macho unaweza kuhama kutoka kwa mmoja kwenda kwa mwingine.

Leo nimeona  nishare na wewe haya machache kuhusu namna ya kulinda macho yako, lakini kwa mawasiliano zaidi wasilina nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 barua pepe ni dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment