Wednesday, 12 August 2015

ZIFAHAMU HIZI SABABU ZA MWANAMKE KUUMWA KIUNO NA TIBA YAKE

Wanawake wengi wamekuwa wakikabiliwa na tatizo la kupata maumivu ya kiuno mara kwa mara na wengi wamekuwa wakiwasiliana nasi kwa lengo la kufahamu sababu hasa ya maumivu hayo.

Miongoni mwa sababu za maumivu ya kiuno ni pamoja na matatizo ya kukosa choo (constipation) matatizo katika mfumo wa uyeyushaji chakula, kukaa vibaya isivyostahili kwa muda mrefu.

Sababu nyingine ni matatizo katika kipindi cha hedhi hii ni moja ya sababu ambayo huchangia tatizo hilo kwa asilimia kubwa zaidi.

Mbali na hizo pia kusimama muda mrefu, kula chakula kisichofaa na unyanyuaji wa vitu vizito nayo ni moja ya sababu.

Unaweza kupoza maumivu hayo kwa kutumia kitunguu swaumu, ambapo utatakiwa kutafuta punje sita za kitunguu hicho na kuziponda kisha utapaka sehemu ya kiuno inayouma kabla ya kulala.

Kwa ushauri au maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment