Monday, 17 August 2015

ZIPATA HIZI SIFA CHACHE ZA MBAAZI


Mbaazi ni mboga ambayo inapatikana sana katika jamii zetu za maisha ya kawaida kabisa, ingawaje mboga hii imeonekana kwamba ni mboga ya watu wa tabaka la chini sana.

Lakini kimsingi mbaazi ni moja ya mboga yenye manufaa sana zaidi ya vile watu wanavyodhani au kufikiri.

Ninazo hapa baadhi ya faida ambazo hupatikana kwa kutumia mbaazi

Husaidia sana kutokuwa na uzito mkubwa, hii ni kutokana na uchache wa kiwango chake cha 'fat'

Pia husaidia sana kurekebisha sukari ya mwili na hivyo kuwasaidia watu wenye shida ya kisukari na kuwafanya kuwa katika hali nzuri.

Husaidia sana kuzuia magonjwa ya moyo pamoja na matatizo ya kukosa choo 'consumption' kwa muda mrefu, tatizo ambalo huwa na madhara kiafya pia.

Mbaazi husaiida kulinda afya ya mifupa, kutokana na kusheheni sana vitamin K

Kwa maelezo na ushauri tupigie simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment