Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 23 September 2015

BAADA YA TAFITI YA TWAWEZA KUTOKA ZITTO KABWE KAYASEMA HAYA KUHUSU UTAFITI HUO


Septemba 22, 2015 Taasisi ya TWAWEZA ilitoa matokeo ya utafiti wao kuelekea uchaguzi Mkuu Oktoba 25, ambapo walibainisha namna ambavyo Watanzani mbalimbali wanamkubali nani zaidi.

Katika matokeo hayo CCM imepata 66%, CHADEMA ikipata 22%, C.U.F 1%,ACT 0%, NCCR 0%, UKAWA 3%.

Sasa baada ya matokeo hayo, Kiongozi wa Chama cha ACT -Wazalendo Zitto Kabwe kupitia Twitter aliandika hivi "Chama chetu kinaamini kwenye tafiti haijalishi zina matokeo mazuri au mabaya kutuhusu, tumepokea matokeo haya kama changamoto… tutaongeza nguvu yetu kuhakikisha tunapata asilimia zaidi kwenye kura"

Hata hivyo Zitto alisema "Ikumbukwe kwamba utafiti huu wa TWAWEZA umefanywa kabla ya chama cha ACT WAZALENDO hakijapata mgombea Urais na kabla ya uzinduzi vilevile"

No comments:

Post a Comment