Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 5 September 2015

BADO HALI SI SHWARI KIPINDUPINDU DAR

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick
Serikali imesema bado hali ni tete ya kumaliza maambukizi ya ugonjwa wa kipindipindu mkoani Dar es Salaam ambao hadi sasa umesababisha vifo vya watu kumi.

Kutokana na hali hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadick amevifungia visima 20 vya maji vilivyobainika kuwa na vimelea vya kipindupindu pamoja na kupiga marufuku uuzaji wa vyakula mashuleni.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Meck Sadick amesema tangu kutokea kwa mlipuko wa kipindupindu, wamepokea wagonjwa 636 katika vituo vya Ilala, Temeke na Kinondoni na kati yao 578 wametibiwa na kuondoka, 90 wanaendelea na matibabu huku 10 wamefariki dunia.

Anasema Manispaa ya Kinondoni imeendelea kuathiriwa na ugonjwa huo, na ameelezea hatua zilizochukuliwa na Serikali kudhibiti maambukizi hayo.

Mbali na hayo, Mkuu wa mkoa huyo akaenda mbali zaidi na kuwataka wanasiasa kuacha mara moja kuhusisha ugonjwa huo na masuala ya kisiasa kwakuwa hayana uhusiano wowote na siasa kwana ni magonjwa kama yalivyo mengine. 


Ugonjwa huo ulijitokeza kwa mara ya kwanza katika maeneo ya Mwananyamala, Manispaa ya Kinondoni ambako kulibainika mgonjwa mmoja na sasa umesambaa katika Manispaa za Ilala na Temeke na kufikia wagonjwa 536

No comments:

Post a Comment