Wednesday, 23 September 2015

DAR INASHIKILIA NAFASI YA SITA KWA MAAMBUKIZI YA UKIMWI AFRIKA


Wakati hali ya maambukizi mapya ya UKIMWI ikipungua nchini, tafiti zimebainisha jijila Dar es Salaam linashikilia nafasi ya sita miongoni mwa majiji yaliyoathurika zaidi barani Afrika.

Takwimu hizi zipo kwenye ripoti ya utafiti uliofanywa na shirika la Wahamiaji (IOM) uliofanywa kwenye bandari ya Dar es Salaam na kuangazia namna jamii za watu wa maeneo ya bandari walivyo nauwezekano mkubwa wa kupata maambukizi mapya ya ugonjwa huo kutokana na muingiliano wa watu wa mataifa mbalimbali.

Mshauri wa mipango wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya UKIMWI (UNAIDS), Marie Engel kayika uwasilishwaji wa ripoti uliofanyika jijini Dar es Salaam alisema ingawa maambukizi yamepungua nchini, bado Dar ni miongoni mwa majiji yaliyoathirika zaidi.

"Dar es Salaam ni jiji la sita kati ya kumi yaliyoathirika zaidi Afrika ikiwa na asilimia 6.2 za maambukizi mapya kwa mwaka. Maambukizi ya ndani yamepungua kwa kiasi na mpaka mwaka jana yalikuwa asilimia tano maeneo ya mjini na 7.2 vijijini, huku wastani kwa nji nzima ikiwa ni asilimia tano" alisema Marie.

Hata hivyo alisema kwamba mapambano dhidi ya ugonjwa huu bado yanaendelea, huku jamii za kimataifa ikiamini ifikapo 2030 ugonjwa huo utakuwa ni historia, licha ya kwamba kuna kazi kubwa inahitajika kufanywa ili kufikia lengo la kuukabili Ukimwi.

Itakumbukwa kwamba ugonjwa wa Ukimwi ulianza kuenea mnamo mwaka 1980


No comments:

Post a Comment