Thursday, 17 September 2015

FAHAMU KUHUSU MBEGU ZA TIKITI MAJI ZINAVYOWEZA KUWASAIDIA WATU WENYE UGONJWA WA FIGO


Figo ni miongoni mwa viungo muhimu sana katika mfumo wa utendaji kazi wa mwili wa binadamu.

Mwili wa binadamu una figo mbili zenye maumbo yanayofanana, lakini kuna wakati figo hupata madhara na kupelekea mhusika kupata ugonjwa wa figo.

Ugonjwa huu wa figo mbali ya kumsababishia maumivu ya hapa na ple mhusika, lakini pia hautibiki kirahisi pamoja na gharama za matibabu yake huwa ni kubwa na wengi kushindwa kuzimudu.

Kuna sababu ambazo huchangia ugonjwa huu miongoni mwa sababu hizo ni pamoja na matumizi holela ya dawa hususani dawa za kutuliza maumivu  na nyinginezo, lakini pia uvutaji wa sigara na unywanji pombe ni mojawapo ya sababu za ugonjwa huu.

Kwa kawaida figo huwa ni muhimu sana ndani ya miili yetu wanadamu kwani husaidia kuchuja vitu mbalimbali ikiwemo sumu katika damu, pamoja na kusaidia kuhifadhi kiwango cha maji na madini mwilini.
Matokeo ya mchujo wa sumu na maji yaliyomwilini ndipo wanadamu huwa tunapata haja ndogo (mkojo).

Magonjwa haya ya figo huweza kujitokeza kwa gafla, lakini kuna wakati tatizo huweza kuanza kujitokeza kwa taratibu, ambapo figo hupoteza kiwango chake cha utendaji kazi polepole.

Zifuatazo ni miongoni kati ya dalili ambazo huashiria kuwapo kwa tatizo katika figo>>>
1. Kwanza mhusika huweza kuanza kupungua kwa kiwango cha haja ndogo (mkojo), kuvimba miguu na wakati mwingine  kushindwa kupumua.

2. Maji kujaa mwilini nayo ni moja ya dalili ya tatizo hili 

3. Mgonjwa pi huweza kuvimba macho na miguu hasa asubuhi

Tazama kipindi cha Mandai afya.com hapa chini umsikilize Tabibu Abdallaha Mandai anavyofafanua kuhusu mbegu za tikiti maji zinavyoweza kuwa tiba ya figo karibu utazame kipindi>>>>Kwa maelezo na ushauri zaidi unaweza kuwasiliana na Tabibu Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.


No comments:

Post a Comment