Tuesday, 15 September 2015

FAHAMU KUHUSU MMEA WA UWATU NA FAIDA ZAKE KIAFYAMmea wa uwatu asili yake ni Ulaya Mashariki , lakini kwa hapa nchini Tanzania mmea huu hustawi zaidi katika visiwa vya unguja na Pemba.

Mmea wa uwatu unavirutubisho vingi ikiwa ni pamoja protini, nyuzinyuzi, madini ya chuma pamoja na calcium.

Majani ya uwatu hutibu matatizo ya mfumo wa chakula hususani tatizo la kutosagika vizuri kwa chakula.

Matatizo mengine ambayo huweza kutibiwa na mmea wa uwatu ni pamoja na shida ya ngozi kuwasha, matatizo ya ini, kuuma kichwa, kukosa choo pamoja na vidonda vya tumbo.

Mbali na hayo pia mmea huu husaidia sana la kunyonyoka kwa nywele, vidonda vya mdomoni majipu na kuvimba mwili.

Pia majani yake yanapopakwa usoni mara kwa mara husaidia sana uso kuonekana vizuri na husaidia kukuza nywele. Halikadhalika husaidia pia kuondoa mikunjo usoni, mba na kumfanya mhusika kuonekana kijana. 


Kwa ushauri na matibabu zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa mawasiliana yafuatayo: 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment