Wednesday, 30 September 2015

FAHAMU KUHUSU SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI


Kwanza kabisa shingo ya kizazi, hii  ni njia ya kizazi kati ya uke na mji wa mimba. Sehemu hiyo ina kazi nyingi ikiwa ni pamoja na kupitisha mbegu za kiume kuelekea katika mirija ya uzazi ili kupevusha yai,.

Kazi nyingine ya shingo ya kizazi ni kupitisha damu ya hedhi na pia ndio mlango anaopitia mtoto wakati wa kuzaliwa. 

Saratani ya shingo ya kizazi ni mabadiliko ya chembe chembe hai zilizo juu au zinazofanana na shingo ya uzazi, lakini kwa mujibu wa watalaam huainisha kuwa saratani hiyo ya shingo ya kizazi husababishwa na kuanza ngono mapema katika umri mdogo chini ya miaka 18.

Pia saratani hiyo huweza kutokea kwa  kuwa na wapenzi wengi na kuvuta sigara. Pia miongoni mwa mambo yanayochangia kupata saratani ya shingo ya kizazi ni pamoja na historia ya kubeba mimba nyingi na unywaji pombe kupindukia huku watu walioathirika na virusi vya Ukimwi wakiwa katika hatari zaidi ya kupata maradhi hayo.

Hata hivyo, kimsingi ugonjwa huu husababishwa na virusi vinavyoitwa Human papilloma, ambapo mtu anaweza kupatwa na virusi hawa wakati wa kujamiana na mtu mwenye maambukizi. 

Miongoni mwa dalili ambazo huashirira tatizo hili ni pamoja na kutokwa na damu ambayo si ya hedhi, kutokwa na uchafu, majimaji au usaha sehemu za siri.

Dalili nyingine ni kuhisi maumivu makali wakati wa kujamiiana na kusababisha kutokwa na damu baada ya tendo hilo, pia maumivu hayo huweza kuambatana na maumivu ya tumbo chini ya kitovu sambamba na maumivu ya kiuno.

Ili kuepuka tatizo hili ni vyema kujenga utaratibu wa kwenda kuchunguza afya mara kwa mara angalau mara moja kila mwaka siku zote wahenga husema kinga ni bora kuliko tiba, basi tufahamu kuwa kwa kujikinga tunaweza kujiepusha na magonjwa mengi na hata haya ya saratani. 

Njia nzuri ya kuepukana na magonjwa haya ni pamoja na kujichunga kitabia na kutofanya ngono zembe.

Kwa ushauri zaidi piga simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment