Wednesday, 9 September 2015

FAHAMU NAMNA MDALASINI UNAVYOWEZA KUSAIDIA TATIZO LA KUPATA HEDHI NDEFU


Habari za leo mdau wa www.dkmandai.com bila shaka ni mzima wa afya kama utakuwa unatatizo basi pia nikupe pole sana.


Kuna maswali nimeendelea kupokea karibu kila siku na nimekuwa nikiyajibu kupitka tovuti yetu hii ya Mandai Herbalist Clinic na leo ninapenda kujibu swali ambalo limekuwa likiulizwa na kinamama wengi kuhusu kupata hedhi kwa muda mrefu.

Kwanza kabisa kwa kawaida mzunguko wa hedhi huchukua siku 21 mpaka 35, na mwanamke huingia kwenye hedhi kwa muda wa siku 3 mpaka 7. 


Na tunaposema mwanamke anapata hedhi ndefu au kwa muda mrefu zaidi ni endapo itatokea mwanamke akiingia kwenye hedhi kwa zaidi ya siku 7. Hali ambayo kitaalamu huitwa menorrhagi.

Tatizo hili huweza kusababishwa na mabadiliko ya homoni au maswala ya matumizi ya njia mbalimbali za uzazi wa mpango, ingawaje si wote huweza kuwasababishia tatizo hili.

Pia tatizo hili la kupata hedhi kwa muda mrefu huweza kusababishwa na maambukizi kwenye via vya uzazi au kuwa na uvimbe kwenye kuta za mji wa uzazi.

Sababu nyingine huweza kuwa ni dalili za mirija ya uzazi kuziba au kiashiria cha tatizo la saratani ya mji wa uzazi

Hata hivyo, ni vizuri kuonana na wataalam wa afya unapoona tatizo hili kwani linaweza kuleta madhara ya kiafya na kijamii,

Mfano wa madhara ya kijamii ni pale ambapo mwanamke atashindwa kabisa kufanya shughuli zake za kimaendeleao, lakini kuhusu madahara ya kiafya ni pamoja na mwanamke kupelekea kupata upungufu wa damu kutokana na kupoteza damu nyingi.

Sasa ili kusaidika na tatizo hili unaweza kutumia mdalisini kwa kupata kijiko kimoja cha unga wa mdalasini kisha changanya kwenye maji (baridi) na ukoroge vizuri , baada ya hapo utatumia mchanganyiko huo asubuhi, mchana na jioni kwa wiki nzima.

Lakini pia unaweza kupata kikombe kimoja cha maji ya moto yenye mchanganyiko wa unga wa mdalasini na kuongeza asali kidogo kisha utakuwa unakunywa asubuhi, mchana na jioni hadi utakapoona mabadiliko.

Unaweza kuwasilina na Tabibu Abdallaha Mandai kwa namba za simu zifuatazo 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment