Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 7 September 2015

FAHAMU NAMNA YA KUEPUKANA NA UNENE KUPITA KIASI

Habari za Jumatatu ya Septemba 07, 2015 msomaji wangu wa www,dkmandai.com bila shaka unaendelea vyema kabisa, lakini kama haupo vizuri napenda kukupa pole sana.

Leo nimeona nizungumzie namna ya kupunguza unene kutokana na kupokea maswali ya watu wengi wakiomba wakiomba kufahamu ni kwa namna gani wataweza kumaliza shida ya unene kupita kiasi.

Hivyo nimeona leo nianze na hili swala la ulaji ambalo wengi wamekuwa wakishindwa kulielewa vyema

 ULAJI.
Ipo mifumo miwili ya kula, yaani chakula unachokula na namna unavyokila.

Unavyokula: Kula vyakula vidogovidogo vyenye madini, vitamin, mafuta nk mara nyingi kwa siku  au kula milo michache  (mmoja au miwili) mkubwa ili kujaza tumbo.

Unapokula mlo mdogomdogo husaidia afya na kuingia mwilini vyema kuliko ulaji mkubwa wa mara chache. ulaji mdogomdogo unaosambazwa mara kadhaa kwa siku ni bora maana mwili huchambua kila kitu kwa wepesi na haraka.

Jinsi ya kula vizuri
Aubuhi kunywa maji kwanza, matunda kisha ndio chai na vitu vingine kama makate au maandazi. 
Baadhi ya watu wanada kwamba wanakula matunda na mboga, tatizo ni kwamba mipangilio yao huwa na makosa, mathalani wengi hula matunda mara baada ya chakula, vimeng'enya chakula  (enzymes) tumboni hufanya kazi kwa namna tofauti, Mathalani vinavyonyambua matunda ni tofauti na vinavyomeng'enya vitu vugumu zaidi kama nyama au wanga.

Matunda hunyambuliwa haraka zaidi kuliko vyakula vingine, hivyo ni bora kula matunda dakika 10 hadi 20 kabla ya chakula . Ukila baadaye matunda hugeuzwa aina fulani ya pombe inayoelea tu juu ya chakula na kubaki kitu kingine badala ya kuingizwa haraka ndani ya damu kupitia utumbo mdogo,

Tatizo jingine ambalo hujitokeza ni kupika mboga hadi zikapoteza nguvu. Mseto wa vyakula pia ni muhimu. Kwa mfano vyakula vyenye uchachu (acid) na vile vinavyomumunyuka haraka havipaswi kuliwa kwa pamoja.

Matunda machachu kama machungwa, mannasi na maembe yanatakiwa yawe pamoja na yale laini zaidi: ndizi mbivu, matikiti maji, mapapai, matufaha nk yaende kivyake maana yana mfumo tofauti wa kumeng'enywa.

Unaweza kuwasiliana na Tabibu Abdalaha Mandai kwa msaada zaidi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment