Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 2 September 2015

FAHAMU NAMNA YA KUKABILIANA NA 'ALLERGY'

Si ajabu ajabu kumsikia mtu akilalamika kuwa akila baadhi ya vyakula anavimba, anawashwa au akisikia harufu ya baadhi ya vitu au manukato na madawa, basi hujikuta anakosa kupumua vizuri, yote hayo kwa ujmla wake huweza kutokea na tunaweza kusema ni mzio 'allergy.'

Mzio au allergy ni ile hali ya mwili kukutana na kitu nje au ndani ya mwili na hatimaye muathirika kujikuta akipiga chafya, kukohoa, kupumua kwa tabu na hata kutapika au kuharisha n.k.

Kimsingi ni kwamba kitu kimoja kinaweza kusababisha  athari za aina tofauti kwa watu tofauti, hii inamaana kwamba kuna mtu anaweza kutumia chakula fulani na kisiweze kumpatia tabu, lakini mtu mwingine anaweza kula chakula hicho hicho na akajikuta akipata baadhi ya madhara.

Sasa kama wewe ni miongoni mwa wale ambao wanasumbuliwa na shida ya mzio unaweza kutumia tiba hii kwa ajili ya kujisaidia ukiwa hapo nyumbani kwako. Unachopaswa kufanya ni kukamua nusu ndimu ndani ya glasi moja ya maji ya uvuguvugu. kisha kunywa kila asubuhi kwa siku tatu.

Unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800. Barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment