Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 7 September 2015

FAHAMU SABABU ZA KUWASHWA SEHEMU ZA SIRI NA NAMNA YA KUEPUKA TATIZO HILI

Habari za leo mdau wa www.dkmandai.com, leo napenda kuzungumzia hili tatizo la kupata muwasho sehemu za siri.

Tatizo hili limekuwa likiwasumbua wanawake wengi na baadhi yao wamekuwa wakiwasiliana nasi kuomba ushauri juu ya tatizo hilo, hivyo leo nadhani ni vyema tukalizungumzia kidogo.

Kimsingi ni kwamba kuwashwa sehemu za siri husababishwa na maambukizi ya fangasi na maambukizi mengine ya bakteria watokanao na kujamiana, lakini wakati mwingine huweza kuwa sababu tofauti na hiyo kama alegi.

Mfano kupatwa na muwasho ndani ya uke (vagina) huweza kusababishwa na matumizi ya kemikali, sabuni zilizowekewa dawa ya kuua bakteria

Aidha, wanawake ambao wameacha kuingia kwenye hedhi wanaweza kupata muwasho kutokana na kubadilika ya kiwango cha homoni, kwani kwa kipindi hicho kuta za uke huwa nyembamba na kukauka na hivyo kupelekea kupata muwasho. 


Zifuatazo ni njia za kuepukana na tatizo hili:

Epuka kufanya ngono zembe.

Jikaushe vizuri maji sehemu za siri mara baada ya kuoga.

Epuka kuvaa nguo za ndani zenye kubana sana

Hakikisha sehemu zako za siri ni safi muda wote.

Epuka kuvaa nguo zenye unyevunyevu

Usishinde kutwa nzima na nguo moja ya ndani ni vyema ukawa unabadilisha kila baada ya mda.

Acha kutumia pads au sabuni zenye dawa na harufu kali.

Mara baada ya haja ndogo uu kubwa ni vyema ukajitawaza kutokea mbele kuelekea nyuma ili kuzuia bakteria wa kwenye njia kubwa ya choo kuingia kwenye uke (vagina)

Ikiwa tayari unasumbuliwa na shida hii kwa muda mrefu na umetumia dawa bila mafanikio jitahidi uwasiliane nasi Mandai Herbalist Clinic kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment