Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 22 September 2015

FURAHA YANGU NIKUONA UNAKUWA NA AFYA NZURI KUPITIA VYAKULA VYETU, LEO NAKUPA HIZI FAIDA ZA KOROSHO

Habari za Jumanne ya leo mdau wangu wa www.dkmandai.com sina sha unaendelea vyema na mihangaiko ya kimaisha, lakini pamoja na kuwa na mihangaiko ya kimaisha afya zetu nazo ni muhimu pia na ndio maana kila siku nakupa elimu kuhusu tiba.

Leo ninazo sifa kadhaa za korosho, Korosho ni moja ya zao la biashara ambalo hupatikana sana Kusini mwa Tanzania, Mtwara, licha ya kwamba zao hili linafahamika sana kama zao la biashara, lakini bado zao hili lina faida kwa afya zetu pia.

Napenda kuchukua muda wako kwa sasa ili niweze kukuelekeza baadhi ya faidi za matumizi ya korosho kama ifuatavyo:

Matumizi ya korosho yanasifika sana kwa kuwa na uwezo wa kulinda afya ya moyo kutokana na kwamba korosha ndani yake inakirutubisho kiitwacho 'antioxidants'

Aidha korosho pia inasifika kwa kuwa na madini ya magnesium ambayo husaidia kuimarisha afya ya mifupa na meno, lakini pia humsaidia mhusika anayependelea kutumia korosho kuwa na nafasi ndogo ya kupatwa na matatizo ya shinikizo la damu, hususani shinikizo la juu la damu.

Pia ulaji wa korosho husaidia sana kuimarisha afya ya usingizi na kumfanya mhusika kuacha kupata usingizi wa mang'amng'am na badala yake atajikuta akipata usingizi mzuri kabisa.

Mara nyingi kinamama wanaoingia kwenye kufungu hedhi 'menopause' wao huzongwa sana na tatizo la kukosa usingizi, hivyo wanashauriwa kutumia korosho ili kuepuka tatizo hilo.

Usisite kuwasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai kwa maelezo zaidi kuhusu magonjwa na jinsi ya kutumia mimea tiba na vyakula pia wasiliana naye kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment